



Baada ya kutoa sare na Ngorongoro Heroes, Azam FC leo imepata ushindi wa 2-1 dhidi ya timu ya Ruvu Shooting katika uwanja wa Ruvu Mkoani Pwani.
Azam FC ilianza kupata goli la kwanza dakika ya 15 ya mchezo lililofungwa na mchezaji John Bocco baada ya kuunganisha krosi ya Faraji Hussein.
Goli hilo lilidumu kwa dakika 20, baada ya beki wa kutumainiwa wa Azam FC, Aggrey Morice kuandika goli la pili kwa mpira wa kichwa baada ya kuunganisha mpira wa adhabu ndogo uliyopigwa kiufundi na Ibrahim Mwaipopo.
JKT walipata penati katika dakika za mwisho kipindi cha kwanza lakini golikipa mpya wa Azam Jackson Chove aliokoa
Matokeo hayo yalizipeleka timu zote mbili mapumziko, huku Azam FC ikiongoza kwa 2-0.
Kipindi cha pili tiu Azam FC ilifanya mabadiliko kuimarisha ngome yake kwa kumtoa Erasto Nyoni na Seleman Kassim ‘Selembe’ na nafasi zao zikachukuliwa na Salum Swed na Jamal Mnyate.
Dakika ya 51 Ruvu Shooting walipata goli kupitia kwa mchezaji Salum Kimai baada ya kuachia shuti lililotinga wavuni na kumuacha kipa wa Azam FC, Jackson Chove akishangaa.
Goli hilo lilileta mabadiliko ya mchezo kwani timu zote zilicheza kwa kukamiana huku Ruvu Shooting wakitaka ushindi katika mechi yao ya nyumbani, na Azam wakiitaji kulinda lango wasipoteze mechi ya leo.
Katika mechi hiyo ya kirafiki, golikipa Jackson Chove alipewa kadi nyekundu baada ya kumkanyaga mchezaji Paul Ndauka na mchezaji wa Ruvu Shooting Gido Chawala alipewa kadi nyekundu baada ya kumsukuma Chove baada ya kumfanyia madhambi Ndauka.
Kocha wa Azam FC,Itamar Amorin amesema kikosi chake kimebadilikana kuimarika kuliko walipokuwa wakicheza mechi yao ya kwanza.
“Timu imecheza vizuri, kuna mabadiliko makubwa hasa upande wa pasi, ball position na ball control ukilinganisha na mechi iliyopita, kwani wameimarika zaidi.” Alisema Itamar.
Ameongeza amerekebisha makosa yaliyotokea katika mechi dhidi ya Ngorongoro, na kuifanya timu hiyo kuwa katika hali nzuri zaidi.
Akizungumzia uwanja wa Ruvu, Itamar alisema ni uwanja mzuri, una nyasi nzuri lakini zimezidi sana na hazifai kwa kuchezea mpira kwani mpira unakwama mara na kupoteza pasi za wachezaji.
Azam FC, Jackson Chove/David Mwasongwe, Ibrahim Shikanda/Malika Ndeule, Mau Bofu, Agrey Morice, Erasto Nyoni/Jamal Mnyate, Ibrahim Mwaipopo, Faraji Hussein/Ally Mkuba, Ramadhani Chombo ‘Ridondo’, John Bocco/Ally Manzi, Mrisho Ngassa/Cosmas Lewis, Seleman Kassim/ Jamal Mnyate.
Yonatus Mbalimo, Mangasin Mbomus, Peter Moses, George Akitenda, George Osey, Owen Mikumba, Godo Chawala, Faraji Makumbo, Martin Lupati, Salum Chimai, Revocatus Maliwa.
Picha hizi zinaonesha maendeleo ya ujenzi wa kituo cha michezo cha Azam FC ambapo kwa mujibu wa Ramani ya Ujenzi kutakuwa na Bwawa la kuogelea la kiwango cha Olympic, hostels za wachezaji, kiwanja cha mazoezi cha nyasi bandia kama kile cha Karume, kiwanja cha mazoezi kingine cha nyasi za kawaida kama za uwanja mpya wa Taifa na uwanja mkubwa wa michezo.
Ujenzi wa kituo hiki unafanywa kwa Awamu ambapo awamu ya kwanza inahusisha hostels za wachezaji, kiwanja cha mazoezi cha nyasi bandia, bwawa la kuogelea, kanteen ya chakula na Uzio wa eneo lote.
Azam Kuwa na Uwanja wake
Habari kwa hisani ya gazeti na Mwananchi
KLABU ya Azam imetangaza kikosi chake na kuweka bayana ujenzi wa uwanja wao kisasa huko Chamanzi Jijini Dar es Salaam na kuhaidi kuanza kutumia kwenye michezo yake ya Ligi Kuu katika mzunguko wa pili.
Klabu hiyo itakuwa ya kwanza hapa nchini kujenga uwanja wa kisasa ambao utakuwa ukitumika kwenye michezo ya Ligi Kuu.
Mwenyekiti wa Azam, Said Mohamed alisema kuwa tayari wameshaingia mkataba na kampuni moja iliyopo Afrika Kusini kwa ajili ya kujenga uwanja huo kwa kutumia nyasi za bandia.
Alisema mbali na nyasi hizo wameshaanza ujenzi wa hosteli za wachezaji wao ambazo zitatumika kama kambi ya wachezaji na zitaanza kutumika rasmi mzunguko wa pili ya Ligi Kuu Tanzania bara unaoanza Agosti 21.
Pia, kambi hiyo itakuwa na kila kitu ambacho ikiwemo sehemu ya kufanyia mazoezi ya viungo ( GYM) ambayo itatumika kwa wachezaji wao kufanya mazoezi ya viungo.
Kwa upande wa wachezaji wanaowaacha mwenyekiti huyo alisema kuwa timu yao imesajili 22 na vijana chini ya miaka 20 sita.
Wachezaji walioacha ni Chrispine Wadenya, Hadid Mhana, Maridad Haule, Nsa job, Said Swed, Salum Machaku, Yahaya Tumba, Ben Kalama, Shaban Kisiga na Dan Wagaluka.
Waliowasajili wapya kwa ajili ya msimu ujao ni Mohamed Binslum, Jackson Chove, Jabil Azizi, Mrisho Ngassa, Kali Ongala ( GIF Sweden) Mutesa Patrick (APR Rwanda) na Ssenyonjo Peter (Polisi Uganda).
Kocha wa timu hiyo Amorian Itamaa alisema kuwa kuacha kwa wachezaji hao wameangalia vitu vingi ikiwemo nidhamu na kushuka kwa uwezo wake uwanjani.
Alisema kunabaadhi ya wachezaji wamekuwa na nidhamu mbaya katuika kambi na mazoezini na wengine wameshuka uwezo ndio maana tumewaacha katika usajili wetu mpya.
Aidha alisema kuwa mchezaji yoyote yule hawe na jina hasiwe na jina kama hatakuwa na midhamu mbaya atawajibishwa kwani msimu huu wamejipanga kuchukua ubingwa wa ligi kuu.
Hata hivyo wachezaji wote waliosajiliwa na klabu hiyo wameingia kambini katika ufukwe wa Bamba beach uliopo Kigamboni nje kidogo ya Dar es Salaam.
ikiwa imesalia siku moja kufikia mwisho wa usajili kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu utakaoanza August mwaka huu, uongozi wa Azam FC umetangaza kukamisha usajili wake na kuanza kwa maandalizi kwa ajili ya ligi hiyo.
Makamu Mwenyekiti wa Azam FC, Said Mohamed amesema usajili wa mwaka huu wameacha wachezaji kumi waliokuwepo msimu ulipita na kubakisha wachezaji 14, huku wakisajili wachezaji wapya nane na kupandisha jumla ya wachezaji sita kutoka katika timu ya vijana 'Azam Academy'.
“Katika usajili wetu tumesajili wachezaji watatu kutoka nje ya Tanzania na watano kutoka katika vilabu vya hapa nchini, tumezingatia taratibu za TFF kwa kusajili wachezaji wa kigeni wasiozidi watano, ni matumaini yetu wachezaji wetu watafanya vizuri” alisema Mohamed.
Mohamed aliongeza kuwa Azam itakuwa na jumla ya wachezaji watano wa kigeni baada ya kuongeza wachezaji watatu ambao wataungana na wengine wawili walipo katika timu hiyo.
Uongozi umewataja wachezaji wapya waliosajiliwa na timu hiyo kuwa ni Mohamed Binslum (Huru) Jackson Chove(JKT Ruvu), Jabir Aziz na Ramadhan Chombo 'Redondo' (Simba), Mrisho Ngassa (Yanga), Kalimangonga Sam Daniel Ongala Rampling 'Kali Ongala' (GIF-Sweeden), Patrick Mutesa Mafisango (APR- Rwanda) na Peter Senyonjo (Polisi-Uganda.)
Wachezaji waliobaki ni John Bocco, Erasto Nyoni, Jamal Mnyate, Salum Aboubakar 'Sure Boy', Vladmir Niyonkuru, Philip Alando, Luckson Kakolaki, Malika Ndeule, Aggrey Morice, Salum Swed, Ibrahim Shikanda, Ally Manzi, Seleman Kasim 'Selembe' na Ibrahim Mwaipopo.
Makamu Mwenyekiti aliongeza kuwa timu hiyo haikuwaacha mbali wachezaji wao wa timu ya vijana 'Azam Academy', imepandisha wachezaji sita ambao ni Sino Augustino, Himid Mao, Mau Ali, Tumba Swed, Ali Mkuba na Samih Nuhu.
Mohamed aliwataja wachezaji walioachwa kuwa ni Chrispin Odula, Habib Mhina, Maridad Haule, Nsa Job, Said Swed, Salum Machaku, Yahya Tumbo, Ben Kalama, Shaaban Kisiga na Dan Wagaluka.
Azam kambini Bamba beach Kigamboni.
Timu ya Azam FC kesho inataraji kuweka kambi Bambabay maeneo ya Kigamboni jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya maandalizi ya ligi kuu.
Azam FC ikiwa kambini itakuwa ikifanya mazoezi mara mbili kwa siku, asubuhi itakuwa ikitumia uwanja wa Uhuru na jioni kufanya mazoezi katika viwanja vilivyopo Kigamboni.
“Tumeamua kwenda Kigamboni kutokana na kupata eneo zuri kwa ajili ya kambi, pia kuna viwanja vizuri vya kufanyia mazoezi” alisema mwenyekiti wa Azam FC, Said Mohamed.
Aliongeza kuwa timu itakuwa huko kwa muda maalum huku ikisubiri taarifa maalum kutoka TFF kama kutakuwa na safari ya kwenda ufaransa, kama haitakuwepo timu itaenda Zanzibar kwa ajili ya maandalizi
Wachezaji wapya
Mohamed Binslum (Huru)
Jackson Chove(JKT Ruvu)
Jabir Aziz na Ramadhan Chombo 'Redondo' (Simba)
Mrisho Ngassa (Yanga)
Kalimangonga Sam Daniel Ongala Rampling 'Kali Ongala' (GIF-Sweeden),
Mutesa Mafisango (APR- Rwanda
Peter Senyonjo (Polisi-Uganda.)
Wachezaji waliobaki
John Bocco,
Erasto Nyoni
Jamal Mnyate
Salum Aboubakar 'Sure Boy'
Vladmir Niyonkuru
Philip Alando
Luckson Kakolaki
Malika Ndeule
Aggrey Morice
Salum Swed
Ibrahim Shikanda
Ally Manzi
Seleman Kasim 'Selembe'
Ibrahim Mwaipopo
Waliopandishwa Kutoka Azam Academy
Sino Augustino
Himid Mao
Mau Ali
Tumba Swed
Ali Mkuba
Samih Nuhu
walioachwa
Chrispin Odula
Habib Mhina
Maridad Haule
Nsa Job
Said Swed
Salum Machaku
Yahya Tumbo
Ben Kalama
Shaaban Kisiga
Kutoka mazoezini leo, tovuti imegundua kuwa wachezaji wapya waliojiunga na timu ya Azam FC wanafanya vizuri hali iliyompa matumaini kocha Itamar Amorin.
Azam FC imefanya usajili kwa kuongeza wachezaji wapya ili kuimarisha kikosi hicho ambacho kina malengo ya kuwa nafasi ya juu katika ligi kuu ijayo.
Wachezaji wapya walikuwepo mazoezini leo ni Mrisho Ngassa, Ramadhani Chombo 'Ridondo', Jackson Chove, Mohamed Slum, Kally Ongala na Jabir Aziz.
Ikiwa ni mara ya kwanza kwa timu tatu bora za ligi kuu ya Tanzania kupata mualiko wa kufanya mazoezi nchini Ufaransa, Timu ya Azam FC imepata nafasi hiyo na kuichukulia kama sehemu yao ya mafanikio.
Kocha Itamar Amorin amesema jitihada walizofanya msimu uliopita ndizo zilizopelekea timu kuwa nafasi ya tatu na kupata mualiko huo wa kwenda Ufaransa.
“Tulikuwa na malengo ya kuwa katika nafasi ya nne lakini tulipoongeza bidii katika mazoezi na mechi zetu tukafanikiwa kuwa katika nafasi ya tatu ambayo imetuwezesha kupata nafasi ya kuwa mmoja ya waalikwa wa kwenda Ufaransa, kama tusingekuwa hgrkatika nafasi ya tatu tusingepata mualiko huo.” alisema Itamar.
Aliongeza kuwa kama timu itapata uthibitisho rasmi wa kwenda Ufaransa, itatumia safari hiyo kama sehemu ya majaribio kama ilivyo katika program ya mazoezi ya kujiandaa na ligi kuu ijayo.
Itamar alisema kuwa mipango ya kufanya mechi za majaribio ikiwa ni sehemu ya maandalizi itategemea na safari ya kwenda Ufaransa kama safari haitaingiliana na siku za mechi za majaribio, kutakuwa na mechi hizo.
Msimu mpya na mambo mapya, Azam FC wameanza mazoezi wakiwa na jezi mpya tofauti na zile walizokuwa wakizitumia msimu ulipoita.
Azam ya sasa ikiwa mazoezini inavaa jezi zenye rangi ya bluu iloyoiva yenye rangi ya chungwa mabegani, huku wakitumia kaptura nyeusi zilizo na mchirizi wa rangi ya chungwa, namba za wachezaji na maandishi ya Azam yanarangi ya chungwa.
Makocha msimu huu wanavaa jezi nyeupe zenye mistari miwili ya rangi za blu pembeni, huku kaptura zao zikiwa nyeupe na mistari miwili ya rangi za blu, jezi hizo zina maandishi yenye rangi za chungwa.
Msimu uliopita Azam FC walikuwa wakitumia jezi zilizokuwa katika mfumo wa Tshirt zenye rangi ya chungwa, na makocha walikuwa wakivaa jezi za rangi nyeupe na bluu bahari.
Timu ya Azam siku ya Jumamosi itakuwa ikifanya mechi yake ya mazoezi dhidi ya timu ya taifa ya vijana chini ya miaka ishirini U20, Ngorongoro Heroes, katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Ikiwa ni mechi ya kwanza ya majaribio kwa timu ya Azam FC, itatumia fursa hiyo kuwapa mazoezi Ngorongoro Heroes ambao wapo katika maandalizi ya kucheza mechi yakufuzu kucheza fainali za Afrika kwa vijana dhidi ya Ivory Coast mwishoni mwa mwezi huu.
Kocha Itamar amesema, mechi hiyo itakuwa muhimu pia kwa timu ya Azam ambayo itakuwa ikifanya maandalizi kwa ajili ya safari ya Ufaransa na ligi kuu ijayo.
“Ngorongoro ni timu imara na nzuri, italeta ushindani mkubwa kwa Azam kwani ina majaribio yake ya kwanza kwa yatakayosaidia kujua uwezo wa timu mapema ili kurekebisha sehemu zitakazokuwa na mapungufu.” aliongeza Itamar.
|
PAMOJA na kupokea kipigo cha kusikitisha cha mabao 4-1 kutoka kwa Ujerumani, England wamemshutumu mwamuzi Jorge Larrionda wa Uruguay aliyekata bao la kusawazisha wakati shuti la kiungo wao Frank Lampard lilipopiga mwamba wa juu na kuanguakia ndani ya mstali.
Bao hilo lilikataliwa na mwamuzi Jorge Larrionda wa Uruguay ikiwa muda mfupi baada ya England kupata bao la kwanza huku Ujerumani ikiongoza kwa mabao mawili, ambapo hata mwamuzi msaidizi Pablo Fandino hakuona mpira kama ulikuwa umevuka mstali wa goli.
Bao hilo lililokataliwa lilipoonyeshwa kwenye marudio ya televisheni ilionekana mpira huo ulivuka mita moja ya mstali wa goli.
Alikuwa ni Frank Lampard ambaye alipiga shuti hilo akiwa mita 40 ambapo kipa wa Ujerumani, Manuel Neur alishindwa kulizuia.
Bao hilo lililokataliwa linafananishwa na bao la tatu la England ambalo lilifungwa na Geoff Hurst mwaka 1966 katika fainali dhidi ya Ujerumani magharibi wakati huo, ambapo wajerumani wanapinga bao hilo halikuvuka mstali na linajadiliwa mpaka leo,katika mechi hiyo England ilishinda 4-2.
Akilizungumzia bao la jana, mwamuzi wa zamani wa Ujerumani Helmut Krug aliiambia televisheni ya Ujerumani kwa England wamekataliwa bao.
"Hilo ni kosa ambalo haliwezi kusameheka, mwamuzi msaidizi alitakiwa kuona, mpira ule ulivuka mstali, mwamuzi msaidizi alitakiwa kuona bila hata ya kurudia kutazama tukio hilo,"alisema Helmut Krug.
Rais wa Shirikisho la soka la Ujerumani Theo Zwanziger aliongeza kwenye mahojiano na televisheni ya Ujerumani wakati wa mapumziko kwamba mwamuzi alitakiwa kuona mpira umevuka mstali pale pale alipokuwepo.
"Tunatakiwa tusimamie sheria za soka tulizonazo, ninaweza kuona kwamba mashabiki wa soka wa England hawakufurahia maamuzi ya mwamuzi kukataa bao, niliweza kuona mpira ule uliingia golini,"alisema Zwanziger.
Tukio hilo litakuwa limechochea uhasama wa timu hizo pinzani England na Ujerumani, pia linatarajiwa litachochea kuanzisha mjadala kwa FIFA kuanza kutumia teknolojia ya video ili kuweza kuwasaidia waamuzi kutatua kutoa maamuzi katika mazingira magumu.
Katika mchezo huo mshambuliaji chipukizi Thomas Mueller alifunga mabao mawili pekee yake baada ya Miroslav Klose na Lukas Podolski kuifungia Ujerumani mabao mawili Ujerumani.
England ilipata bao lake la kufutia machozi lililofungwa na beki Matthew Upson katika dakika 37 England kabla ya bao la Lampard kukataliwa dakika moja baadaye.
JENGO LAU 11
DAKAR; Watu 11 wamepoteza maisha kaskazini mwaSenegal baada ya jengo walilokuwa wamekaa na kuangalia mechi za Kombe la Dunia kuanguka ghafla katika mji wa Matam uliopo kaskazini mwa Darak.
Tukio hilolilitokea wakati mashabik hao wakishudia mechi kati ya Uruguay dhidi ya Korea Kusini.
APS ilimkariri afisa usalama akisema watu wengine wawili wameumia vibaya baada ya kudondokewa na jengo hilo.
Senegal haijafuzu kwa fainali za Kombe la Dunia mwaka huu, lakini mashindano hayo yamekuwa yakiwavuta watu wengi na kufutilia kupitia vituo mbalimbali vya televisheni.