Sunday, June 27, 2010

Ambani amtabiria makubwa Ngasa


MSHAMBULIAJI wa Yanga, Boniface Ambani amewataka wanachama na mashabiki wa timu hiyo kumpa ushirikiano kiungo mshambuliaji wa Azam FC, Mrisho Ngassa kama alivyokuwa akiitumikia klabu yao.

Ambani ambaye yupo nchini Kenya kwa ajili ya mapumziko ameliambia Championi Ijumaa kuwa, Ngassa asionekane kama msaliti baada ya kutimkia Azam, kwa kuwa viongozi wa timu hiyo walishindwa kumtekelezea mahitaji yake.

kwa mujibu wa gazeti la Champion, “Hakuna mchezaji asiyeipenda klabu yake milele, ni vema mashabiki wakatambua hilo, wanaotakiwa kutupiwa lawama ni viongozi ambao kama wangekuwa na nia ya kumhitaji aendelee kuichezea klabu hiyo naamini wangeweza kumbakisha kwa kiasi chochote.

“Pia itambulike soka ni sehemu ya maisha, kipindi ambacho mchezaji anawika ndiyo hicho cha kukitumia kuliko kuendelea kuchezea timu kwa mapenzi siyo kwa ajili ya maisha ya baadaye,” alisema Ambani ambaye naye amekuwa akihusishwa na mipango ya kuhamia Azam.

Katika msimu wa 2008/2009 Ambani alitwaa tuzo ya ufungaji bora, lakini aliiachia tuzo hiyo msimu uliopita na kwenda kwa Mussa Mgosi.

No comments:

Post a Comment