Sunday, June 27, 2010

kumbe Nadir Haroub Canavaro yupo huru

WACHEZAJI Mussa Hassani ‘Mgosi’ wa Simba na Nadir Haroub ‘Cannavaro’ wa Yanga ni miongoni mwa wachezaji 38

wa Simba na Yanga ambao wapo huru kwa kuwa wamemaliza mikataba yao inayotambuliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Ofisa Habari wa TFF Florian Kaijage jana alitangaza orodha ya wachezaji 155 wa timu mbalimbali ambao ama wametemwa au wamemaliza mikataba yao katika klabu tisa kati ya 12 zitakazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao.

Katika orodha hiyo ya wachezaji waliomaliza mikataba yapo majina ya Mgosi na Haroub, ambapo awali ilinukuliwa na viongozi wa klabu hizo kongwe nchini kuwa wachezaji hao bado wana mikataba halali na klabu hizo, hivyo hawezi kujiunga na klabu nyingine pasipo kufanya mazungumzo.

Mbali na Mgosi na wachezaji wengine waliomaliza mikataba yao kwa Simba ni Ramadhani Chombo na Jabir Aziz ambao tayari wamejiunga na klabu ya Azam, Mohamedi Banka, Salum Kanoni, Juma Jabu, Kelvin Yondani, Juma Nyoso,Nico Nyagawa, David Naftali na Mohamedi Kijuso.

Wengine ni Haruna Shamte, Adam Kingwande, Ulimboka Mwakingwe, Salim Aziz, George Nyanda, Ally Mustapha, Meshack Abel na Deo Munishi.

Kwa upande wa Yanga wachezaji waliomaliza mikataba yao mbali na Cannavaro ni kipa Obren Cuckovic, Shadrack Nsajigwa, Nurdin Bakari, Abdi Kassim, Godfrey Bonny, Bakari Mbegu, Moses Odhiambo, Kabongo Honore, Boniface Ambani, Hamisi Yusuf, Fred Mbuna,Vicent Barnabas na Ally Msigwa.

Klabu ya Yanga imetangaza kuwatema wachezaji wake Amir Maftah na Mcameroun Robert Mba kwa madai ya utovu wa nidhamu ndani ya klabu hiyo.

Mgosi na Cannavaro wamekuwa wakihusishwa kutaka kujiunga na Azam ya Dar es Salaam.

Katika orodha hiyo wachezaji 23 wa Mibwa wamemaliza mikataba yao, ambapo timu nyingine na idadi ya wachezaji waliomaliza mikataba katika mabano ni Majimaji (25),Toto Afica (9), Kagera Sugar (26), Azam (17), JKT Ruvu (9),African Lyon(8).

Kwa upande wa Azam wachezaji wake waliomaliza mkataba na klabu hiyo imetangaza haitaongeza ni Habibu Mhina, Crispine Odula, Maridadi Haule, Nsa Job, Osborne Monday, Said Sued, Salum Machaku, Yahya Tumbo, Ben Kala na Shaaban Kisiga.

Wachezaji waliomaliza mikataba yao na wapo huru ni Vladmir Niyonkuru, Ibrahim Mwaipopo, Ibrahim Shikanda, Dan Wagaluka, Luickson Kakolaki, Erasto Nyoni na Philip Alando.

No comments:

Post a Comment