Saturday, June 26, 2010

Redondo: Nitawaonyesha kaziREDONDO amesema kuondoka Simba kumemfanya awe huru zaidi na atacheza soka la hali ya juu msimu ujao zaidi ya lile lililoonekana Msimbazi.

Mchezaji huyo aliyemaliza mkataba na Simba amejiunga na Azam kwa mkataba wa miaka miwili lakini akasisitiza kuwa bado mpango wake wa kwenda Al-Hodood ya Misri uko palepale.

"Msimu ujao nitafanya kazi kwa uhuru sana, naamini nitacheza soka sana kuliko nilivyokuwa Simba, haimaanishi kuwa siku huru mwanzoni lakini maisha ya huku yananifanya niongeze nguvu sana,"alisema Redondo ambaye jina lake halisi ni Ramadhani Chombo.

"Nimekutana na changamoto mpya na mategemeo ni makubwa sana hasa kutokana na Azam ilivyo na aina ya wachezaji iliyowasajili, naamini tutacheza mpira sana na mimi nitakuwa mmojawapo.

"Nimesaini mkataba mrefu lakini endapo dili yangu ya Misri ikikaa vizuri nitakwenda nimewaambia viongozi wangu na wamenielewa,"alisisitiza mchezaji huyo aliyewahi kuchezea Ashanti United iliyoshuka daraja.

No comments:

Post a Comment