Tuesday, July 13, 2010

Kama safari ya Ufaransa ipo, basi ni matunda ya jitihada zetu


Ikiwa ni mara ya kwanza kwa timu tatu bora za ligi kuu ya Tanzania kupata mualiko wa kufanya mazoezi nchini Ufaransa, Timu ya Azam FC imepata nafasi hiyo na kuichukulia kama sehemu yao ya mafanikio.

Kocha Itamar Amorin amesema jitihada walizofanya msimu uliopita ndizo zilizopelekea timu kuwa nafasi ya tatu na kupata mualiko huo wa kwenda Ufaransa.

“Tulikuwa na malengo ya kuwa katika nafasi ya nne lakini tulipoongeza bidii katika mazoezi na mechi zetu tukafanikiwa kuwa katika nafasi ya tatu ambayo imetuwezesha kupata nafasi ya kuwa mmoja ya waalikwa wa kwenda Ufaransa, kama tusingekuwa hgrkatika nafasi ya tatu tusingepata mualiko huo.” alisema Itamar.

Aliongeza kuwa kama timu itapata uthibitisho rasmi wa kwenda Ufaransa, itatumia safari hiyo kama sehemu ya majaribio kama ilivyo katika program ya mazoezi ya kujiandaa na ligi kuu ijayo.

Itamar alisema kuwa mipango ya kufanya mechi za majaribio ikiwa ni sehemu ya maandalizi itategemea na safari ya kwenda Ufaransa kama safari haitaingiliana na siku za mechi za majaribio, kutakuwa na mechi hizo.

No comments:

Post a Comment