Thursday, July 15, 2010

Ngasa Hajaacha pengo, asema papic


Habari kwa hisani ya Habari leo

KOCHA Mkuu wa Yanga Kostadin Papic amesema aliyekuwa mshambuliaji wa timu hiyo Mrisho Ngasa hajaacha pengo katika timu hiyo, ila ameacha nafasi, ambayo imeshazibwa.


Papic akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mazoezi ya timu hiyo katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam jana, alisema.

Ngasa ameacha nafasi ambayo imeshazibwa na wachezaji wengine na sio pengo kama wengi wanavyodhania.

Papic alisema kimsingi nafasi ya mchezaji huyo imejazwa na wachezaji Shamte Ally, Nsa Job na Kenneth Asamoah ambao anaamini wanaweza kuisaidia Yanga kama alivyofanya Ngasa.

Mshambuliaji Kenneth Asamoah alisaini kuichezea Yanga akitokea nchini Ghana wakati Nsa Job amejiunga na klabu hiyo baada ya kutupiwa virago na timu yake ya zamani ya Azam FC.

Ally alikuwepo Yanga wakati wa Ngasa. Papic alisema kwamba kimsingi timu haiwezi kuundwa kwa kumtegemea mchezaji mmoja bali mchezaji mmoja anaweza kuwa sehemu ya timu.

Ngasa winga hatari wa klabu hiyo alisaini mkataba wa miaka mitatu kuichezea Azam, uhamisho uliogharimu Sh milioni 58.

No comments:

Post a Comment