Thursday, July 15, 2010

Mambo ya Chamazi












Picha hizi zinaonesha maendeleo ya ujenzi wa kituo cha michezo cha Azam FC ambapo kwa mujibu wa Ramani ya Ujenzi kutakuwa na Bwawa la kuogelea la kiwango cha Olympic, hostels za wachezaji, kiwanja cha mazoezi cha nyasi bandia kama kile cha Karume, kiwanja cha mazoezi kingine cha nyasi za kawaida kama za uwanja mpya wa Taifa na uwanja mkubwa wa michezo.

Ujenzi wa kituo hiki unafanywa kwa Awamu ambapo awamu ya kwanza inahusisha hostels za wachezaji, kiwanja cha mazoezi cha nyasi bandia, bwawa la kuogelea, kanteen ya chakula na Uzio wa eneo lote.



Azam Kuwa na Uwanja wake

Habari kwa hisani ya gazeti na Mwananchi

KLABU ya Azam imetangaza kikosi chake na kuweka bayana ujenzi wa uwanja wao kisasa huko Chamanzi Jijini Dar es Salaam na kuhaidi kuanza kutumia kwenye michezo yake ya Ligi Kuu katika mzunguko wa pili.

Klabu hiyo itakuwa ya kwanza hapa nchini kujenga uwanja wa kisasa ambao utakuwa ukitumika kwenye michezo ya Ligi Kuu.

Mwenyekiti wa Azam, Said Mohamed alisema kuwa tayari wameshaingia mkataba na kampuni moja iliyopo Afrika Kusini kwa ajili ya kujenga uwanja huo kwa kutumia nyasi za bandia.

Alisema mbali na nyasi hizo wameshaanza ujenzi wa hosteli za wachezaji wao ambazo zitatumika kama kambi ya wachezaji na zitaanza kutumika rasmi mzunguko wa pili ya Ligi Kuu Tanzania bara unaoanza Agosti 21.

Pia, kambi hiyo itakuwa na kila kitu ambacho ikiwemo sehemu ya kufanyia mazoezi ya viungo ( GYM) ambayo itatumika kwa wachezaji wao kufanya mazoezi ya viungo.

Kwa upande wa wachezaji wanaowaacha mwenyekiti huyo alisema kuwa timu yao imesajili 22 na vijana chini ya miaka 20 sita.

Wachezaji walioacha ni Chrispine Wadenya, Hadid Mhana, Maridad Haule, Nsa job, Said Swed, Salum Machaku, Yahaya Tumba, Ben Kalama, Shaban Kisiga na Dan Wagaluka.

Waliowasajili wapya kwa ajili ya msimu ujao ni Mohamed Binslum, Jackson Chove, Jabil Azizi, Mrisho Ngassa, Kali Ongala ( GIF Sweden) Mutesa Patrick (APR Rwanda) na Ssenyonjo Peter (Polisi Uganda).

Kocha wa timu hiyo Amorian Itamaa alisema kuwa kuacha kwa wachezaji hao wameangalia vitu vingi ikiwemo nidhamu na kushuka kwa uwezo wake uwanjani.

Alisema kunabaadhi ya wachezaji wamekuwa na nidhamu mbaya katuika kambi na mazoezini na wengine wameshuka uwezo ndio maana tumewaacha katika usajili wetu mpya.

Aidha alisema kuwa mchezaji yoyote yule hawe na jina hasiwe na jina kama hatakuwa na midhamu mbaya atawajibishwa kwani msimu huu wamejipanga kuchukua ubingwa wa ligi kuu.

Hata hivyo wachezaji wote waliosajiliwa na klabu hiyo wameingia kambini katika ufukwe wa Bamba beach uliopo Kigamboni nje kidogo ya Dar es Salaam.


1 comment:

  1. I wish Mungu azidi kumuongezea huyu mja wake na ipo siku Said Bakhresa aanze kujenga Hospitali na kuweka madaktari bingwa.
    Ni kheri mtu kulipa zaidi ukapata huduma nzuri kuliko huu uozo tulionao.

    Hongera sana Azam Company haya ndiyo maendeleo nchini.
    Ajira za kumwaga. Alhamdulillah.

    ReplyDelete