Sunday, June 27, 2010

England out, waishia kulilia goli laLampard

PAMOJA na kupokea kipigo cha kusikitisha cha mabao 4-1 kutoka kwa Ujerumani, England wamemshutumu mwamuzi Jorge Larrionda wa Uruguay aliyekata bao la kusawazisha wakati shuti la kiungo wao Frank Lampard lilipopiga mwamba wa juu na kuanguakia ndani ya mstali.

Bao hilo lilikataliwa na mwamuzi Jorge Larrionda wa Uruguay ikiwa muda mfupi baada ya England kupata bao la kwanza huku Ujerumani ikiongoza kwa mabao mawili, ambapo hata mwamuzi msaidizi Pablo Fandino hakuona mpira kama ulikuwa umevuka mstali wa goli.

Bao hilo lililokataliwa lilipoonyeshwa kwenye marudio ya televisheni ilionekana mpira huo ulivuka mita moja ya mstali wa goli.

Alikuwa ni Frank Lampard ambaye alipiga shuti hilo akiwa mita 40 ambapo kipa wa Ujerumani, Manuel Neur alishindwa kulizuia.

Bao hilo lililokataliwa linafananishwa na bao la tatu la England ambalo lilifungwa na Geoff Hurst mwaka 1966 katika fainali dhidi ya Ujerumani magharibi wakati huo, ambapo wajerumani wanapinga bao hilo halikuvuka mstali na linajadiliwa mpaka leo,katika mechi hiyo England ilishinda 4-2.

Akilizungumzia bao la jana, mwamuzi wa zamani wa Ujerumani Helmut Krug aliiambia televisheni ya Ujerumani kwa England wamekataliwa bao.

"Hilo ni kosa ambalo haliwezi kusameheka, mwamuzi msaidizi alitakiwa kuona, mpira ule ulivuka mstali, mwamuzi msaidizi alitakiwa kuona bila hata ya kurudia kutazama tukio hilo,"alisema Helmut Krug.

Rais wa Shirikisho la soka la Ujerumani Theo Zwanziger aliongeza kwenye mahojiano na televisheni ya Ujerumani wakati wa mapumziko kwamba mwamuzi alitakiwa kuona mpira umevuka mstali pale pale alipokuwepo.

"Tunatakiwa tusimamie sheria za soka tulizonazo, ninaweza kuona kwamba mashabiki wa soka wa England hawakufurahia maamuzi ya mwamuzi kukataa bao, niliweza kuona mpira ule uliingia golini,"alisema Zwanziger.

Tukio hilo litakuwa limechochea uhasama wa timu hizo pinzani England na Ujerumani, pia linatarajiwa litachochea kuanzisha mjadala kwa FIFA kuanza kutumia teknolojia ya video ili kuweza kuwasaidia waamuzi kutatua kutoa maamuzi katika mazingira magumu.

Katika mchezo huo mshambuliaji chipukizi Thomas Mueller alifunga mabao mawili pekee yake baada ya Miroslav Klose na Lukas Podolski kuifungia Ujerumani mabao mawili Ujerumani.

England ilipata bao lake la kufutia machozi lililofungwa na beki Matthew Upson katika dakika 37 England kabla ya bao la Lampard kukataliwa dakika moja baadaye.

JENGO LAU 11
DAKAR; Watu 11 wamepoteza maisha kaskazini mwaSenegal baada ya jengo walilokuwa wamekaa na kuangalia mechi za Kombe la Dunia kuanguka ghafla katika mji wa Matam uliopo kaskazini mwa Darak.

Tukio hilolilitokea wakati mashabik hao wakishudia mechi kati ya Uruguay dhidi ya Korea Kusini.

APS ilimkariri afisa usalama akisema watu wengine wawili wameumia vibaya baada ya kudondokewa na jengo hilo.

Senegal haijafuzu kwa fainali za Kombe la Dunia mwaka huu, lakini mashindano hayo yamekuwa yakiwavuta watu wengi na kufutilia kupitia vituo mbalimbali vya televisheni.

No comments:

Post a Comment